Sunday, April 15, 2012

Muheza Hospice Care yatimiza miaka 10

Muheza Hospice Care ni taasisi ya kibinafsi ambayo ilianzishwa mnamo mwaka 2001 kwa lengo la kuhudumia wagojwa wenye maradhi ya kusendeka yaani yasiyotibika kama vile Saratani, kisukari, UKIMWI na kadhalika.
Tiba hii kwa wagonjwa walio na maradhi ya kusendeka huitwa TIBA SHUFAA au palliative care, mfumo wa utoaji tiba ni tofauti na tiba nyingine kwani tiba hii hutolewa na timu maalumu yenye wataalamu mbalimbali kama vile madaktari, manesi, maafisa jamii, viongozi wa dini, viongozi wa kisiasa hususani katika ngazi ya kijiji/kitongoji na wengineo.
tarehe 31 March 2012, Muheza Hospice Care iliazimisha miaka 10 tangu kuanzishwa kwake, mgeni wa heshima katika hafla hiyo alikuwa Mhashamu Baba Askofu wa dayosisi ya Tanga ya Kanisa la Kianglikana Familia ya karolyn na Richard Collins ni moja kati ya waanzilishi wa Muheza Hospice Care, nao walijumuika katika sherehe hizo za miaka kumi.
 Ngoma za asili zilikuwepo pia katika kuipamba hafla hiyo.
 Maandamano yaliongozwa na Matarumbeta toka kanisa la kilutheri Muheza
 Meza kuu: Kushoto ni Mwenyekiti wa Halmashauri mheshimiwa kiroboto, akifuaitiwa na Mhashamu askofu, pamoja na mganga Mfawidhi wa Hospitali Teule.
 Mganga Mfawidhi akijiandaa kumkaribisha mgeni rasmi
 Baadhi ya wageni waalikwa na katikati ni kwaya ya Kanisa la Anglikani-Muheza
 Mhashamu Baba askofu akinukuu masuala muhimu yatokanayo
 Hata watoto pia walijumuika katika hafla hiyo muhimu.
 Kwaya ya kanisa la Angilikani ikitumbuiza
  Sehemu ya umati wa wageni waalikwa ambao walhudhuria
 Mwenyekiti wa Muheza Hospice Care akiongoza zoezi la kufungua Champagne
 Mhashamu askofu akianza kutoa hotuba yake
 Keki mahsusi ambayo iliandaliwa kwa hafla hiyo
 Mwenyekiti wa Muheza Hospice Care na Karolyn wakijiandaa kukata keki.
 Hapa wanajadili mkakati wa kukata keki hiyo
 Mwenyekiti anatangaza mkakati huo
 Waalikwa toka TPCA na wizara ya Afya walikuepo pia
 Baadhi ya wana washiriki wakijiandaa kufungua champagne
 Mhashamu Askofu akihutubu katika hafla hiyo
 Mhashamu Askofu aliendesha Harambee ya kuchangia watoto waishio mazingira hatarishi ambao wanahudumiwa na Hospice.
 Zoezi la harambee likiendelea kwa umakini mkubwa
 Baadhi ya washiriki wa hafla hiyo wakiendelea kuchangia
 Mhashamu Askofu akitoa zawadi kwa watumishi waliotukuka
 Dada Mary Kauki mmoja kati ya waanzilishi akipokea zawadi yake
 Huyu nae akijongea jukwaa tayari kupokea zawadi yake
 Kwa heshma na taadhima akipokea zawadi yake

 Msafara wa maandamano katika maadhimisho hayo
Maandamano yakiendelea

2 comments: